RAS MSOVELA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA USHAURI MKOA WA SHINYANGA...ATOA MAAGIZO KUHUSU WANAFUNZI 7,416 AMBAO HAWAJARIPOTI SHULE

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, akizungumza kwenye kikao cha kamati ya ushauri Mkoa wa Shinyanga

Na Marco Maduhu, Shinyanga.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, ameendesha kikao cha kamati ya ushauri Mkoa wa Shinyanga (RCC), ambapo taarifa mbalimbali za utekelezaji zimewasilishwa.

Kikao hicho kimefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, na kuhudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wenyeviti wa Halmashauri, Maofisa kutoka Taasisi za Serikali, Katibu wa Mbunge Jimbo la Shinyanga Mjini, pamoja na viongozi wa dini.

Aidha kwenye kikao hicho limezungumziwa suala la Elimu, Afya, Kilimo cha Pamba, Upandaji miti, Maji,Umeme, Mindombinu ya barabara, Madini, na hali ya uchumi.

Akizungumza kwenye kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela amesema kikao hicho ni muhimu sana kwa mustakabali wa maendeleo ya mkoa wa Shinyanga.

Akizungumzia suala la elimu, amewataka Wakurugenzi, Maofisa elimu na watendaji wote kwenye sekta hiyo hadi kufikia Machi mwaka huu awe ameshapewa taarifa za wanafunzi 7,416 ambao walichaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu na hawajaripoti shule.

Amesema katika mkoa huo wafunzi 26,217 walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, lakini walioripoti shule ni 19,776, huku 7,416 bado hawajaripoti katika shule walizopangiwa.

"Natumia fursa ya mkutano huu kutoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri, Ofisa Elimu wa Mkoa na Halmashauri, na watendaji wengine wa Serikali kuhakikisha hadi kufikia mwenzi Machi niwe nimepata taarifa za wanafunzi hawa 7,416 ambao hawajaripoti shule," alisema Msovela.

Pia amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kusimamia kikamilifu zoezi la ujenzi wa vyumba vya madarasa ili vijengwe kwa kiwango bora kuendana na thamani ya fedha, pamoja kukamilika ndani ya muda uliotolewa na Waziri Mkuu mwisho Februari 28 mwaka huu.

Aidha katika Kilimo cha zao la Pamba, amewataka Maofisa ugani, kutembelea wakulima na kutoa elimu ya kilimo cha kisasa pamoja na kuwasambazie mbegu za kutosha la zao hilo.

Pia amesisitiza suala la upandaji miti, kuwa wananchi wahamasishwe kupanda miti kwa wingi ili kuifanya Shinyanga kuwa ya kijani.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akichangia mada kwenye kikao hicho kwa upande wa kilimo, amewataka maofisa ugani watekeleze wajibu wao wa kutoa elimu ya kilimo cha kisasa kwa wananchi, ambapo wana lalamikiwa sana na wakulima kutotoa elimu hiyo ya kilimo bora.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba, akichangia mada kwenye suala la elimu, amesema wao kishapu wanajipanga zaidi kujenga madarasa mengi ambapo wamejiwekea malengo ya kujenga vyumba vya madarasa 122.

Pia akizungunzia suala la wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya CHF iliyoboreshwa, ametoa ushauri elimu iendelee kutolewa zaidi kwa wananchi, pamoja na uboreshaji wa utoaji huduma za matibabu kwa wananchi wenye bima za afya.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, akizungumza kwenye kikao cha kamati ya ushauri Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye kikao cha kamati ya ushauri Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabanga Talaba, akizungumza kwenye kikao cha kamati ya ushauri Mkoa wa Shinyanga.
Katibu tawala msaidizi mipango na uratibu mkoani Shinyanga Joachim Otaru, akiwasilisha taarifa za mipango na bajeti za mwaka Mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Ofisa Elimu Mkoa wa Shinyanga James Malima, akiwasilisha taarifa za elimu mkoani humo, kwenye kikao hicho cha kamati cha ushauri mkoa.
Meneja wakala wa maji vijiji (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Shinyanga kwenye kikao hicho cha RCC.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga DK, Nuru Mpuya, akiwasilisha taarifa ya sekta ya afya kwenye kikao hicho.
Katibu tawala uchumi na uwezeshaji Mkoa wa Shinyanga Beda Chamatata,akiwasilsiha taarifa ya kilimo cha zao la Pamba kwenye kikao hicho.
Mhandisi kutoka Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga Anthony Tarimo. akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Shirika kwenye kikao hicho.
Dk. Deogratius Macha Meneja idara ya uchumi kutoka Benki kuu Tawi la Mwanza, akiwasilisha taarifa ya hali ya uchumi.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba, kushoto, akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kwenye kikao cha kamati ya ushauri Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wa kamati wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wa Kamati wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wa Kamati wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wa Kamati wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wa Kamati wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wa Kamati wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wa Kamati wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wa Kamati wakiwa kwenye kikao.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Shinyanga George Mrutu, akichangia mada kwenye kikao hicho.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samwel Jackson, akichangia mada kwenye kikao cha kamati ya ushauri Mkoa wa Shinyanga RCC.
Mkuu wa chuo cha ufundi Stadi Veta mkoani Shinyanga Mangu Mabelele, akichangia mada kwenye kikao hicho cha RCC.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post