MREMBO AGANDISHA NYWELE ZAKE KWA GUNDI KIMAKOSA....HALI NI TETE, SASA ATAKA AOMBEWE TU


Mwanamke mmoja wa Louisiana amefika hospitali kutafuta tiba baada ya kujipulizia gundi kwenye nywele kwa bahati mbaya badala ya mafuta ya kawaida ya nywele.

Taarifa kuhusu mkasa wa nywele uliompata Tessica Brown, ulifahamika mapema mwezi Februari baada ya kusema kuwa amekuwa akiweka mtindo mmoja wa nywele kwa muda wa mwezi mmoja bila kubadili kwasababu alijipaka gundi badala ya mafuta na jitihada zake za kuosha nywele ziligonga mwamba.

"Nywele zangu haziwezi kuchanika au hata kuvutika.Nimeosha nywele zaidi ya mara 15 lakini hakuna mafanikio yoyote ziko vilevile." alisema kwenye mtandao wake wa Instagram.

Kwa mujibu wa tovuti ya Gorilla Glue , wameandika gundi ambayo aliitumia haiwezi kutoka kwa maji kwa asilimia 100% na matumizi yake ni kugundisha marumaru za bafuni na paa.

Kampuni hiyo iliposikia mkasa uliomkuta mwanamke huyo walimtumia ujumbe kwenye Twitter wakimuomba radhi kwa kile kilichomtokea.

Jumamosi, Bi. Brown,alipiga picha tena na kuweka kwenye mitandao ya kijamii kuwajulisha wafuasi wake kuwa hamna mabadiliko yoyote katika nywele zake.

Aliweka picha akijaribu kuzinyofoa nywele zake.

Baada ya kutoka hospitalini alishukuru kila mtu na kuwaomba waendelee kumuombea kuweza kukabiliana na changamoto inayomkabili.

Kampuni ya gundi imesemaje ?
Gorilla Glue imemwambia bi. Tessica kuwa kesi yake ni ya kipekee maana bidhaa yao si ya kuweka kwenye nywele hivyo wanadhani hakuna kitu anachoweza kukifanya kubadili hali iliyomkuta.

Kampuni hiyo ilimpa pole kwa kukutwa na tukio hilo na wanamtakia kila la kheri katika matibabu yake.

Walisema hawana cha kusema bali kumpa pole na hawashauri mtu yeyote kutumia bidhaa yao kwenye nywele. Na kama mtu akitumia na kujaribu kuziosha kwa sabuni au pombe anaweza kupata madhara mengine.

Gorilla Glue iliandika kabisa kuwa si kwa matumizi ya nywele.

Maelezo ya onyo katika bidhaa zao ni muhimu sana na wateja wanapaswa kuzingatia suala hilo.

Gundi yao ni kwa ajili ya kugundisha vitu kama makaratasi ,mbao, nguo lakini si nywele.


Hali yake ikoje sasa?
Kwa mujibu wa taarifa ya TMZ , imeeleza kuwa kampuni ya Gorilla Glue ni kama dada huyo ataenelea kuishi wakati nywele zikiwa zimegundika na hakuna suluhu la tatizo lake , wamesema hata akienda mahakamani hana kesi ya kuwashitaki.

Mmoja wa wanafamilia ameeleza bado Bi.Brown anaendelea kupata matibabu.

Tessica tayari ameanzisha harambee za kuomba msaada wa malipo ya hospitali ... Mpaka sasa amepokea dola $9,000 kwa ajili ya matibabu na watu bado wanatuma.

Gharama ya matibabu yake mpaka sasa yanaweza kumgharimu zaidi ya $12,000.
 
CHANZO - BBC SWAHILI

Soma pia

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post