PIPI MAHABA ZA KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA KWA WANAWAKE ZAZUA GUMZO , MADAKTARI WAONYA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, February 17, 2021

PIPI MAHABA ZA KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA KWA WANAWAKE ZAZUA GUMZO , MADAKTARI WAONYA

  Malunde       Wednesday, February 17, 2021


Wakati matangazo ya vipipi vya kuongeza uwezo na hamu ya kushiriki tendo la ndoa yakizidi kushamiri mitandaoni, madaktari wameonya matumizi ya bidhaa hizo na nyingine zinazodaiwa kuwasaidia wanawake.

Siku za karibuni kumekuwapo na matangazo yanayonadi pipi hizo maarufu kama ‘pipi mahaba’ ambazo pia zinauzwa kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya wanawake, zikiwamo saluni.

Mamlaka za Serikali, ikiwamo Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Baraza la Tiba Asili na Tiba mbadala na taasisi hizi zote zimeeleza kutozifahamu pipi hizo wala zinavyotengenezwa.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Mwananchi hivi karibuni umebaini kuwa wanawake wanazichangamkia pipi hizo zinazodaiwa kusaidia kuongeza uwezo, hamu ya kushiriki tendo la ndoa na kumfurahisha mwanaume.

Pipi hizo zenye rangi nyeupe mithili ya maji zimekuwa habari ya mjini kwa sasa, kuanzia mitandaoni hadi katika maeneo yenye mikusanyiko ya wanawake.

Kulingana na wauzaji, pipi hizo ni suluhisho la matatizo ya kimwili yanayoweza kumletea vikwazo mwanamke katika ushiriki wake kwenye tendo la ndoa.

Via Mwananchi


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post