RAIS MAGUFULI ATANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO KIFO CHA MAALIM SEIF SHARIF HAMADRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.

Taarifa ya Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa Maombolezo hayo yameanza Tarehe 17 Februari, 2021 na kwamba bendere zote zitapepea nusu mlingoti.

Taarifa hiyo ya Ikulu pia imeambatana na salamu za pole kwa Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, Familia ya Marehemu na watanzania wote.

“ Nimepokea kwa Masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mhe. Malim Seif Sharif Hmad aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar. Natoa pole kwa Rais wa Zanzibar Mhe.Dkt. Mwinyi, Fmilia, wazanzibarwanachama wa ACT-Wazalendo na Watanzania wote. Mungu amuweke mahala pema peponi, Amina”.Amesema Mhe. Rais Magufuli

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post