NYUKI WA AJABU WAZUA BALAA MAKABURINI..WAOMBOLEZAJI WAKIMBIA JENEZA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, February 16, 2021

NYUKI WA AJABU WAZUA BALAA MAKABURINI..WAOMBOLEZAJI WAKIMBIA JENEZA

  Malunde       Tuesday, February 16, 2021

Na Rajabu Athumani - Mwananchi
 Ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Daudi Mohamed wakazi wa kata ya Kileleni wilayani Handeni mkoani Tanga wametimua mbio na kuacha jeneza lenye mwili wake baada ya eneo la makaburi kuvamiwa na nyuki.

Tukio hilo limetokea leo mchana Jumanne Februari 16, 2021 na hadi saa 11 jioni mazishi yalikuwa hayajafanyika

Mmoja wa shuhudia wa tukio hilo, Abdallah Mchakato amesema nyuki hao walikuwepo tangu saa 8 mchana walipofika makaburini kuchimba kaburi lakini walizidi baada ya ndugu na jamaa kufika eneo hilo.

"Mwili tumeuacha imebidi tutimue mbio wale nyuki si wa kawaida, kuna watu wamezidiwa na kudondoka sijui hali zao huko..., mtaa mzima wamejifungia ndani,” amesema.

Mganga mkuu wa hospitali ya mji Handeni, Hudi Shehedadi amesema amepokea watu tisa waliojeruhiwa na nyuki na kwamba wawili walikuwa na majeraha zaidi, “wengine saba walitibiwa na kuruhusiwa.”

Msemaji wa familia, Rashid Kilagula amesema tukio hilo halina uhusiano na imani za kishirikina na kuwataka ndugu, jamaa na marafiki kutokuwa na hofu.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post