MASHIMO TISHIO STENDI YA MABASI MKOA WA SHINYANGA

Madereva,Mawakala wa Mabasi, abiria na wananchi wanaofanya shughuli mbalimbali katika Stendi ya Mabasi Mkoa wa Shinyanga maarufu ‘Manyoni’ iliyopo Ibinzamata Mjini Shinyanga wameziomba Mamlaka zinazohusika kuziba mashimo yaliyopo katika eneo la stendi hiyo.

Wakizungumza na Malunde 1 blog leo Alhamisi Februari4,2021 wamesema mashimo yaliyopo eneo la kuingilia,ndani na eneo la kutokea yamekuwa yakisababisha usumbufu kwa madereva wakikwepa mashimo hayo lakini pia yanaharibu magari na kuwa chanzo cha ajali eneo la stendi.

“Haya mashimo sasa yana zaidi ya miezi sita,mabasi yanalazimika kukwepa mashimo na wakati mwingine yanatumbukia kwenye mashimo na kuharibu Spring, na hali hii kama mamlaka hazitafanyia kazi inaweza kusababisha kutokea ajali”,wamesema.

Pia wamelalamikia uchafu uliopo katika choo cha Stendi ambapo maji machafu yamekuwa yakitiririka
Basi likikwepa mashimo wakati likiingia katika stendi ya Mabasi mkoa wa Shinyanga iliyopo Ibinzamata Mjini Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya mashimo katika eneo la kuingilia mabasi stendi ya mabasi mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya mashimo katika eneo la kuingilia mabasi stendi ya mabasi mkoa wa Shinyanga.
Basi likikwepa mashimo ndani ya stendi ya mabasi mkoa wa Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya mashimo katika eneo la kutokea mabasi stendi ya mabasi mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya mashimo katika eneo la kutokea mabasi stendi ya mabasi mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya mashimo katika eneo la kutokea mabasi stendi ya mabasi mkoa wa Shinyanga.
Moja ya mashimo ndani ya stendi ya mabasi mkoa wa Shinyanga

Picha na Malunde 1 blog



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments