MTOTO WA MIAKA 8 ACHAPWA KWA WAYA AKIPAKWA CHUMVI MAKALIONI KISA KAIBA 1200 | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, February 4, 2021

MTOTO WA MIAKA 8 ACHAPWA KWA WAYA AKIPAKWA CHUMVI MAKALIONI KISA KAIBA 1200

  Malunde       Thursday, February 4, 2021
Na Peter Saramba - Mwananchi
Mtoto mwenye umri wa miaka minane (jina linahifadhiwa) mkazi wa mtaa wa Mission jijini Mwanza anaugulia majeraha kwenye makalio baada ya kuchapwa kwa waya huku akiwa amepakwa chumvi kwa tuhuma za kuiba Shilingi 1200.

Ukatili dhidi ya mtoto huyo anayesoma darasa la pili katika shule ya msingi Sahara jijini Mwanza unadaiwa kutendwa na baba yake mzazi Februari Mosi, 2021.

Mwalimu wa darasa ndiye aliyebaini majeraha ya mtoto huyo kwenye makalio yote mawili baada ya kumtilia shaka kutokana na kuchechemea kila alipotembea.

Akizungumza akiwa chini ya ulinzi, mama wa kambo wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Auliditensia Bwire amesema siku ya tukio, mume wake aliyemtaja kwa jina la Rahman Suleiman alimtuhumu mtoto wake kuiba Sh1, 200 ndipo alipoanza kumchapa huku akimpaka chumvi kwenye makalio.

Via Mwananchi

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post