WATU ZAIDI YA 60 WAFARIKI DUNIA AJALI YA BOTI MTO CONGO

Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamesema zaidi ya watu 60 wamezama baada ya mashua kupinduka na kuzama katika mto Congo.

Watu 300 wameokolewa lakini inakisiwa kuwa watu wengine 200 hawajulikani walipo baada ya ajali hiyo.

Wakazi wanasema boti iligonga mwamba mashariki mwa mji mkuu Kinshasa, wakati walipokuwa wakisafiri usiku, safari za majini nyakati za usiku zimepigwa marufuku nchini humo.

Waziri wa masuala ya kibinadamu, Steve Mbikayi, amewataka wale wamiliki wa boti kushtakiwa.

"Chombo kilichojaa kupita kiasi, kilichokuwa na abiria zaidi ya 700 kilipinduka Mai-Ndombe! Miili 60 tayari imepatikana na watu 300 wamenusurika Tunazipa pole familia zilizofiwa na tunataka hatua zichukuliwa dhidi ya wale wote wanaohusika na sekta ya uchukuzi,"aliandika Waziri huyo kwenye mtandao wa Twitter.

Kuna barabara chache nchini DRC na shughuli nyingi za usafiishaji wa mizigo na abiria hufanywa kwa njia ya mto.

CHANZO - BBC SWAHILI


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post