AMPIGA RISASI MWENZAKE AKIDHANI NI NYANI SHAMBANI


Picha ya nyani mzee
***
 Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mhina Ally (42)  anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Pwani kwa tuhuma ya kumpiga risasi na kumjeruhi mguuni mwenzake Tatu Hassan (55)  mkazi wa Miono wilayani Bagamoyo aliyekuwa analima shambani baada ya kudhani anampiga nyani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema tukio hilo limetokea Jumapili Februari 14,2021 saa 4 asubuhi katika kitongoji cha Mafungo Makao Makuu Chalinze mkoa wa Pwani.

Amesema baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo walikwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake na kukuta akiwa na bunduki mbili aina ya gobore ambazo anazimiliki kinyume cha sheria na kwamba upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post