VIJANA WALILIA AJIRA UJENZI WA DARAJA LA JPM | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, January 13, 2021

VIJANA WALILIA AJIRA UJENZI WA DARAJA LA JPM

  Malunde       Wednesday, January 13, 2021


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, amemtaka Mkandarasi anayejenga Daraja la Magufuli  jijini Mwanza, kutoa ajira nyingi za vibarua kwa vijana wazawa ili wanufaike na mradi huo.

Agizo hilo amelitoa Waziri huyo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo yaliyofikiwa had sasa.

“Miradi yote ambayo tunalipa pesa zetu wenyewe tuhakikishe wakandarasi wazawa wanajumuishwa kwenye kazi, ili kuweza kupata uzoefu kwa vijana wetu wa kitanzania”.amesisisitiza waziri chamuriho

Waziri Chamuriho pia amewataka Bodi ya Wakandarasi nchini (CRB), kuhakikisha inawaongezea uwezo wakandarasi wazawa ili waweze kuwa pamoja katika Miradi mbalimbali ya Ujenzi wa barabara, na madaraja.

“Katika miradi yote mikubwa lazima tuweke asilimia kubwa kwa wakandarasi wazawa ili tuweze kupata wakandarasi wenye weledi”.aliongezea waziri chamuriho

Aidha, Waziri Chamuriho amewapongeza wakandarasi kwa kazi nzuri ya ujenzi wa daraja hilo na kumuagiza mkandarasi wa daraja hilo kuhakikisha anakamilisha mradi huo kwa wakati.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)Mkoa wa Mwanza ,Mhandisi Fedestus Malibe, amesema kuwa Daraja la JPM linajengwa kwa lengo la kuunganisha barabara kuu ya Isagara-sengerema-Geita- katika ziwa Victoria na litakapokamilika litarahisisha usafirishaji baina ya pande zote mbili.

Naye, Afisa Utumishi wa kampuni ya CCE onesphory Ngonyani, amemhakikishia Waziri huyo kuendelea kutoa ajira kwa vijana wazawa wa eneo hilo, hadi pale ujenzi huo utakapokamilika.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post