SERIKALI YAANZA MCHAKATO UJENZI MRADI MKUBWA WA UMEME MTO RUHUJI NJOMBE
Wednesday, January 13, 2021
Timu ya Watalaamu wa Serikali imefika na kufanya ukaguzi wa kwanza katika maporomoko ya mto Ruhuji katika kijiji cha Itipula mkoani Njombe ambao unatarajiwa kujengwa mradi mkubwa wa umeme utakaozalisha megawats 358 za umeme.
Mradi huo ambao utajengwa katika kipindi cha miezi 36 unaotarajiwa kuanza mwezi juni au julai mwaka huu ulifanyiwa utafiti kwa mara ya kwanza 1998 na kisha kusimama kwa muda mrefu jambo ambalo lilisababisha wananchi kupoteza matumaini na kuanza kurudi kwenye maeneo waliotakiwa kupisha.
Naibu katibu mkuu wizara ya nishati mhandisi Leonard Masanja akizungumza mbele ya timu ya watalaamu kutoka wizara ya nishati,TANESCO na wakazi wa vijiji vinavyozunguka eneo la mradi amesema katika mradi huo uliosubiriwa kwa zaidi ya 22 kutajengwa mabwawa 2,Intake moja pamoja miuondombinu ya umeme na barabara.
Tito Muinuka ambaye ni mkurugenzi wa shirika la umeme TANESCO nchini anasema kitendo cha kufika hapo ni mwanzo wa kuanza utekelezaji wa mradi huo na kwamba kukamilika kwake kutaongeza kiwango cha hazina ya megawats nchini huku Wangwe Elieza Mjiolojia wa TANESCO akisema kutajengwa Zanziber DAM ,Storage Dam na Intake moja
Kwa upande wao wakazi wa kijiji cha Itupula na vijiji jirani akiwemo Eleteus Mkolwe,Josphat Mwenda ambao ni miongoni mwa waliosimama kufanya shughuli za mendeleo ya kudumu katika la mradi kwa zaidi ya miaka 22 wanasema wamefurahishwa na uamuzi huo wa serikali na kwamba wana amini wanakwenda kupata ajira kwa vijana kupitia mradi huo
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin