TANGA UWASA YAANDAA MRADI MKUBWA WA KUONGEZA UZALISHAJI WA MAJI KUTOKA LITA ZA UJAZO 30,000 HADI 45,000 KWA SIKU

 

Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Ujenzi wa Mamlaka Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa)Mhandisi Salum Ngumbi akizungumza na wananchi wa mtaa wa Kange Kasera Kata ya Maweni Jijini Tanga  wakati akitoa elimu kwa wananchi wa mtaa wa Kange Kasera Kata ya Maweni Jijini Tanga.
Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Ujenzi wa Mamlaka Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa)Mhandisi Salum Ngumbi akizungumza na wananchi wa mtaa wa Kange Kasera Kata ya Maweni Jijini Tanga wakati akitoa elimu kwa wananchi wa mtaa wa Kange Kasera Kata ya Maweni Jijini Tanga. kulia wa kwanza ni  na anayefuatilia ni Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayalla
Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayalla akieleza jambo wakati wa mkutano huo

Wananchi wa Mtaa wa Kange Kasera Kata ya Maweni wakiwasikiliza wataalamu kutoka Tanga Uwasa
Mkazi wa Mtaa wa Kange Kasera Kata ya Maweni Seba akiuliza swali katika mkutano huo
 

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira  Tanga (Tanga Uwasa )imeandaa mradi mkubwa wa kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita za ujazo 30,000 kwa siku  hadi  kufikia lita 45,000 kwa siku.


Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Ujenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Salum Ngumbi wakati akizungumza wakati akitoa elimu kwa wananchi wa mtaa wa Kange Kasera Kata ya Maweni Jijini Tanga.

Elimu hiyo ambayo ilitolewa wakati wa mkutano huo imekuwa endelevu kuweza kukutana na wananchi kusikiliza kero zao na namna ya kuweza kuzipatia ufumbuzi ambao ulifanyika shule ya Msingi Kasera.

Alisema kwa sasa Tanga Uwasa wanazalisha maji mita za ujazo elfu 30 kwa siku lakini mahitaji ya wananchi kwa siku ni mita za ujazo elfu 35 kwa siku.

“Kutokana na hilo ndio maana tumepanga kufanya mradi wa  kuongeza miuondombinu ya kuzalisha maji kutoka mita za ujazo elfu 30 mpaka elfu 45 kwa siku na mradi huo utaanza mwezi Aprili mwaka huu”Alisema

Mhandisi Salum alisema mradi huo utakuwa wa miezi 12 na utakuwa na manufaa makubwa mawili katika mji wa Tanga la kwanza wananchi upatikanaji wa  maji ya uhakika ambayo hayakatikikatiki na maji yatapatikana maeneo yote masaa 24.

Alisema pia wakati wa utekelezaji mradi vijana watanufaika  kwa sababu watakwenda kuongeza machujio mawili kwenye mtambo wa kusafishia maji uliopo mowe Pande.

Aidha alisema hivyo kazi ya ujenzi kubwa itafanyika na kuna tenki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita milioni 1 na watakwenda kujenga jengine lenye ujazo wa lita milioni 1 eneo la Pande .

Mhandisi huyo alisema pia watalaza bomba kubwa lenye kipenyo cha milimita 600 kwa urefu wa kilomita 12.5 kutoka mowe mpaka Kange Jeshini na kwenye tenki  hilo bomba litakuwa na kazi ya kusafirisha maji wanayoyazalisha na watakiwa na mabomba mawili makubwa ya kupelekea maji Tanga.

“ Hivyo vijana watanufaika kwenye kazi za ujenzi kuchimba mitaro kwani kwenye mikataba ambayo wataingia na wakandarasi  kwamba kazi yoyote ambayo haihitaji wataalamu maalumu inatakiwa itoke sehemu ya mradi kata ya maweni inaguswa kwa eneo la Mkurumuzi mpaka kange Jeshini"Alisema 
 
Aliwataka vijana wajitokeza kwa wingi kupata hiyo ajira ya muda hivyo tunawaomba wananchi kuwa tayari kupokea mradi na kutoa ushirikiana na mradi mkubwa una thaman i ya Bilioni 8.4 na wanasoimamia wenywe wataalamu wa Tanga Uwasa

Awali akizungumza katika mkutano Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayala hivi sasa wamekuwa wakijitahaidi kadri wawezavyo kuboresha huduma zao  na sasa hawana utaratibu mpaka mteja kufika ofisini kwao  wanatumia simu zao wanapata huduma.

Alisema walichokwenda kuzungumza nao leo ni kutambulisha mradi mkubwa wa kutanua mtambo wa kuzalisha na kutibu maji wa Mowe ambapo maeneo yote ya kata za Maweni na Kiomoni yataguswa moja kwa moja na huo mradi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments