MTANGAZAJI MAARUFU LARRY KING AFARIKI DUNIA


Mtangazaji maarufu nchini Marekani Larry King enzi za uhai wake

Mtangazaji maarufu nchini Marekani Larry King amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87 huko Los Angeles.

Larry King alikuwa maarufu kote duniani kwa kipindi chake cha mahojiano

King ameaga dunia Jumamosi katika kituo cha matibabu cha Cedars-Sinai kulingana na Ora Media, kampuni ambayo yeye pia ni mshikiri wa uanzilishi wake.

Wakati wa taaluma yake ya miaka 60, ambayo ni pamoja na miaka 25 ya kuwa mtangazaji wa kipindi chake mwenyewe katika Shirika la CNN, King alihoji viongozi wengi maarufu wakiwemo wanasiasa, wasanii na hata wanamichezo.

Mwezi huu, alitibiwa ugonjwa wa virusi vya corona, vyombo vya habari vya Marekani vimesema.

Miaka ya hivi karibuni mtangazaji huyo amekuwa na matatizo kadhaa ya kiafya ikiwemo mshtuko wa moyo.

King alianza kuwa maarufu miaka ya 1970 kwa kipindi chake cha redio kwa jina 'The Larry King Show', katika uliokuwa mtandao wa redio wa kibiashara wa 'Mutual Broadcasting System'.

Pia alikuwa mtangazaji wa kipindi cha 'Larry King Live' cha CNN kati ya mwaka 1985 na 2010, akihoji watu tofauti tofauti.

Pia aliandikia makala gazeti la USA Today kwa zaidi ya miaka 20.

Hivi karibuni, King alipeperusha kipindi kingine cha, Larry King Now, kupitia mtandao wa Hulu pamoja na kituo cha Televisheni cha kimataifa cha RT kinachomilikiwa na serikali ya Urusi.

CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post