SIMBA SC YAMTAMBULISHA RASMI KOCHA WAKE MPYA...NI MWAMBA HASA WA SOKA!


Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez akimkabadhi jezi ya mabingwa wa nchi Kocha Mkuu mpya Didier Gomes Da Rosa
Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez na Kocha Mkuu mpya Didier Gomes Da Rosa wakisaini mkataba

Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez na Kocha Mkuu mpya Didier Gomes Da Rosa wakionesha mkataba mbele ya waandishi wa habari 
Na Damian Masyenene
BAADA ya kimya cha muda mrefu na usiri mkubwa, hatimaye Wekundu wa Msimbazi Simba SC wamemtambulisha rasmi Kocha wao Mkuu atakayekinoa kikosi hicho kinachokabiliwa na mashindano mbalimbali makubwa ikiwemo kuutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha huyo mpya wa Simba atakayerithi mikoba ya Sven Vandenbroeck ni Didier Gomes Da Rosa raia wa Ufaransa.

Wakimtambulisha leo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mabingwa hao watetezi wa Tanzania wamesema

"Ni Mwamba hasa wa soka la Afrika akiwa na uzoefu mkubwa wa mashindano makubwa katika bara hili, huku akiwa ameshinda mataji kadha wa kadha.

"Mwalimu huyu ana leseni A ya Uefa inayomfanya awe kocha wa daraja la juu duniani. Karibu Simba Kocha Didier na utapata ushirikiano kutoka kwa klabu na Wanasimba wote kwa ujumla. #NguvuMoja,"

Akizungumza mara baada ya kutambulishwa, kocha huyo mpya amesema “Nina furaha sana kuwa hapa na tuna nafasi ya kufanya mengi pamoja mbeleni.”- Kocha Didier baada ya kutambulishwa. Timu niliyoondoka niliamua mwenyewe. Nataka kuwepo Simba kwa muda mrefu.”- Kocha Mkuu mpya, Didier Gomes Da Rosa

Katika hatua nyingine, jana Klabu hiyo ilimtambulisha kocha wao mpya wa makipa kutoka nchini Brazil, Milton Nienov, ambaye amewahi kuwa kocha wa makipa katika klabu za Polokwane City, Lamontville Golden Arrows FC, Super Eagles FC, Free State Stars FC za Afrika Kusini na Club de Regatas Vasco da Gama, Sport Club Recifie na Figueirense FC za Brazil.

CHANZO- SHINYANGA PRESS CLUB BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments