AUAWA BAADA YA KUMFUMANIA MKEWE AKICHEPUKA NA NJEMBA NYINGINE CHUMBANI KWAKE | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, January 7, 2021

AUAWA BAADA YA KUMFUMANIA MKEWE AKICHEPUKA NA NJEMBA NYINGINE CHUMBANI KWAKE

  Malunde       Thursday, January 7, 2021


Mtu aliyetambuliwa kwa jina la Juma Kitemango (48) mkazi wa Matundasi Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya, ameuawa kwa kushambulia na vitu vyenye ncha kali na mgoni wake, Juma Sunzima (40) baada ya kuwafumania na mkewe wakiwa ndani ya chumba chake. 


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Jerome Ngowi,  amewaambia waandishi wa habari Januari 6 jijini humo kuwa tukio hilo lilitokea Januari 4 wilayani humo, baada ya marehemu kufika nyumbani kwake na kumkuta mkewe Merry Daimon, akiwa na mwanaume aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wake. 


"Marehemu aliwafumania mkewe na mtuhumiwa wakiwa wanafanya yao ndani ya nyumba yake waliyokuwa wakiishi na mkewe na ndipo ulipotokea mzozo na mtuhumiwa kumjeruhi na vitu vyenye ncha kali na sehemu za kichwani na utosini na kusababisha kifo chake," alisema.


Asema mara baada ya tukio hilo mke wa marehemu na mtuhumiwa  walikimbia  na kwamba  jeshi la polisi linaendelea na msako ili wafikishwe mikononi mwa sheria.


Alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mareheme kabla ya umauti kumkuta walikuwa na migogoro isiyokwisha na mkewe ya kimahusiano iliyohusihwa na wivu wa kimapenzi.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post