BASATA YAMTAKA DIAMOND PLATINUMZ KUTUMIA WASANII WALIOSAJILIWA KWENYE TAMASHA LAKE

 

Msanii Naseeb Nyange 'Diamond Platinumz

Baraza la Sanaa Taifa ( BASATA ) limewataka wasanii wote ambao watatumbuiza katika Tamasha la ‘Tumewasha’ linaloendeshwa na Wasafi Media kuhakikisha wamesajiliwa na baraza hilo ili kuwa na uhalali wa kupanda jukwaani.
-
Akizungumza na waandishi wa habari hii leo, Mkurugenzi Mtendaji wa ‘Wasafi Media’ Naseeb Nyange ‘Diamond Platnumz’ amesema wako tayari kufuata agizo hilo ili kuepuka kufungiwa kwa tamasha hilo litakalohusisha wasanii wa ndani na nje ya nchi.
-
"Tunatamani kuwa na wasanii wote, hivyo kwa wasanii ambao hawajasajiliwa na Basata wasajiliwe ili tuwe nao” amesema Diamond Platnumz.
-
Kuelekea tamasha hilo litakalofanyika Januari 30, 2020 Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam ‘Diamond’ amesema kuwa wasanii ambao hawajasajiliwa na wako tayari kufanya hivyo atawasaidia kujisajili kupitia tamasha hilo kw angalizo ‘Tumewasha Tour’

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post