RAIS MAGUFULI AITAKA WIZARA YA MADINI KUTOCHELEWESHA MRADI WA UZALISHAJI MADINI YA NIKELI


Rais Dkt John Magufuli amesema hatua ya kusainiwa kwa mradi wa uzalishaji madini ya Nikeli kati ya Serikali na kampuni ya LZ Nickel Limited, inaashiria kuwa sasa Tanzania itaanza kufaidi matunda ya kuwa na madini hayo hapa nchini.

Akihutubia baada ya kushuhudia utiaji saini mkataba wa mradi huo mjini Bukoba mkoani Kagera, Rais Magufuli amesema kuwa Watanzania wamechoka kusubiria mradi huo ambapo tangu mwaka 1976 madini hayo yaligundulika hapa nchini.

Rais Magufuli amesema, Tanzania ni tajiri kwenye sekta ya madini na hivyo ni wakati muafaka sasa kuanza kufaidi matunda ya utajiri huo kwa kutafuta Wawekezaji wenye nia nzuri na maendeleo ya Tanzania.

Akizungumzia mradi huo Rais Magufuli amesema, Madini hayo ya Nikeli yatasaidia ukuaji wa uchumi wa Tanzania hasa kipindi hiki ambacho nchi inatekeleza mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR).

Ameitaka wizara ya Madini kutochelewesha mradi huo na kutoa ushirikiano kwa Wawekezaji hao ili kuharakisha uzalishaji wa madini ya Nikeli yanayotarajiwa kuzalishwa kutoka kwenye mradi wa Kabanga uliopo mkoani Kagera.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments