Maonyesho Ya Nanenane Kitaifa Mwaka 2021 Kufanyika Mkoani Tabora

 Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya anautaarifu umma na wananchi kuwa Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nanenane kwa mwaka 2021 Kitaifa yatafanyika Kanda ya Magharibi Mkoani Tabora katika Viwanja vya Fatma Mwasa vilivyopo eneo la Ipuli. 


Akizungumza na waandishi wa habari jana  ofisini kwake Jijini Dodoma Kusaya amesema maonesho haya yatakuwa ni ya 29 tangu yalipoanza kuadhimishwa mwaka 1993 na kuwa Wizara ya Kilimo inatoa wito kwa wadau wote wa maonesho zikiwemo Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri, Taasisi za umma na binafsi, wakulima, wafugaji, wavuvi na wanaushirika  kuanza maandalizi ya kufanikisha maonesho.


Pamoja na kufanyika kitaifa mkoani Tabora, Maonesho yatafanyika pia kwenye Kanda zingine (7) ambazo ni Kanda     ya Mashariki Uwanja wa Maonesho ya Mwl. Nyerere (Morogoro); Kati (Nzuguni - Dodoma); Kusini (Ngongo – Lindi); Nyanda za Juu Kusini (John Mwakangale – Mbeya); Kanda ya Ziwa Mashariki (Nyakabindi – Simiyu); Kanda ya Ziwa Magharibi (Nyamhongolo –Mwanza), na Kaskazini (Themi – Arusha).

Imetolewa na:
Revocatus A. Kassimba
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments