Tanzia : MTANGAZAJI WA REDIO FARAJA JENNIFER MAHESA AFARIKI DUNIA


Jennifer Mahesa akifurahia jambo enzi za uhai wake
Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa Kituo cha Matangazo Redio Faraja Fm Stereo  ya Mjini Shinyanga Jennifer Paulo Mahesa amefariki dunia leo asubuhi Ijumaa Disemba 4,2020 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Taarifa za kifo cha Jennifer Mahesa zimetolewa na Mkurugenzi wa Radio Faraja Fm Stereo  Padri Anatoly Salawa kwa niaba ya Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu.

"Tunasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi wetu wa Radio Faraja Jennifer Paul Mahesa ambaye alikuwa Mwandishi wa Habari na Mtangazaji ambacho kimetokea leo Ijumaa saa moja na nusu asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu", amesema Padri Salawa.

Amesema kwa mujibu wa taarifa ya Familia ya Jennipher Mahesa mazishi yatafanyika Siku ya Jumamosi Disemba 5,2020 saa 10 jioni Mjini Shinyanga.

R.I.P Jennifer Mahesa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post