KATIBU MTENDAJI WA BASATA GODFREY MNGEREZA AFARIKI DUNIA


Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza amefariki dunia usiku siku ya Disemba 24, huko Jijini Dodoma katika Hospitali ya General ambapo alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.


Taarifa hizo zimethibitishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya BASATA ambaye ametangaza kifo hicho na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi


Ratiba ya mazishi bado haijatolewa ila tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu kukupa kile kinachoendelea kuhusiana na msiba huu.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments