JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAIPONGEZA TANZANIA KWA MIRADI YA KIMKAKATI


 Jumuiya ya Afrika Mashariki imeeleza kujivunia na miradi mikubwa nay a kimkakati inayotekelezwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba kukamilika kwake kutachochea ukuaji wa uchumi na biashara katika Jumuiya hiyo pia kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Eng. Steven Mlote akiwa na ujumbe wa Jumuiya hiyo ameyasema hayo wali potembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere ambalo linatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2022 ambalo litazalisha Migawati 2115 za umeme.

Mhandisi Mlote ameeleza kuvutiwa na taarifa ya mradi huo kufadhiliwa na fedha za Watanzania na kumpongeza Rais Dkt Magufuli kwa maono hayo lakini pia kitendo cha kutoa zaidi ya ajira 5000 ambapo asilimia 90 ni Watanzania. 

Awali ujumbe huo wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki umetembelea mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa lengo la kijionea maendeleo ya ujenzi wa maradi huo na kueleza kufurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli na kuwasihi vijana wa Kitanzania waliopata fursa ya ujenzi wa reli kuendelea kujifunza kwa moyo na kwa kujituma ili kupata maarifa na ujuzi wa kuendelea kutunza, kuendesha na kuendeleza mradi huo hata baada ya wataalmu kutoka kampuni inayohusika na ujenzi kuondoka nchi.

Mhandisi Mlote ametoa wito kwa Watanzania hasa ambao wanazunguka eneo la miradi hiyo kuitunza na kuilinda kwa kuwa manufaa yake ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao shambani na bidhaa za viwandani pia kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na watu ndani ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kati.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments