HATIMAYE TRUMP ASAINI MUSWADA WA MISAADA YA CORONA NA BAJETI YA SHIRIKISHO | MALUNDE 1 BLOG

Monday, December 28, 2020

HATIMAYE TRUMP ASAINI MUSWADA WA MISAADA YA CORONA NA BAJETI YA SHIRIKISHO

  Malunde       Monday, December 28, 2020


Rais wa Marekani Donald Trump hatimaye ameusaini muswada wa sheria wa dola bilioni 900, unaokusudia kutoa misaada kwa watu walioathiriwa na janga la virusi vya corona, pamoja na bajeti ya serikali ya shirikisho ya dola trilioni 1.4. 

Awali, Rais Trump alikataa kutia saini muswada huo tangu ulipopitishwa na bunge wiki iliyopita. 

Kulikuwa na wasiwasi kuwa kuchelewa kufanya hivyo, baadhi ya faida za ukosefu wa ajira zingepotea, na kwamba mamilioni ya watu wanaweza kupoteza pesa katikati mwa ugumu wa kiuchumi uliochangiwa na janga la virusi vya corona.

 Trump alitaka baadhi ya vipengele vya matumizi, ikiwemo misaada ya kigeni kuondolewa katika bajeti. 

Rais huyo hakusema kwanini ameamua kutia saini sheria hiyo lakini saa chache kabla ya kuusaini aliandika katika Twitter kwamba watu watarajie habari njema. 

 

-DWUsikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post