JAJI MKUU WA TANZANIA PROF. IBRAHIM JUMA ATAKA WAHITIMU CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO KUMUDU MATUMIZI YA TEHAMA

Jaji mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma ameutaka Uongozi wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kuhakikisha wahitimu wanaomaliza chuoni hapo kumudu matumizi ya TEHAMA pamoja na kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao ili kuingia katika kazi ya ushindani.

Ameyasema hayo katika mahafali ya 20 chuoni hapo yakiwa yameambatana na maadhimisho ya kilele cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.

Prof.  Ibrahim amesema wanafunzi wanaotokana na chuo hicho lazima wawe wanafunzi wa karne ya 21 na karne ya 21 inaongozwa na wanawake tofauti na karne zilizopita ilikuwa zikiongozwa na wanaume.

Hivyo amewataka wajaribu kuwapandisha wanafunzi wa astashahada na stashahada ili wawe sambamba na mapinduzi makubwa yanayoendelea katika matumizi ya tehama katika huduma mbalimbali.

"Wahitimu wenu lazima wafahamu namna kanuni za ufunguaji wa mashauri kwa njia ya elecronic zinazotumika kila siku mahakamani ili wawe wanafahamu namna gani tehama inatumika mahakamani", alisema Prof. Ibrahim.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa chuo Dkt. Gerald Ndika amesema tafiti mbalimbali za wataalamu wa uchumi duniani zinaonyesha kuwa nchi ambazo uchumi wake umekua kwa kiasi ni nchi ambazo zimewekeza zaidi kwenye maarifa na ujuzi.

Amesema chuo kimeendea kufanya vizuri katika technolojia ya habari ya mawasiliano TEHAMA kwa kuakisi hilo chuo kimeendelea kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kimataifa ikiwemo taasisi ya mafunzo na utafiti ya umoja wa mataifa (United Nations Institute For Trainning and Research -Unitar) iliyopo Uswisi.

Pia Dkt. Ndika ameeleza kuwa zimekuwepo juhudi zinazofanywa na uongozi wa chuo katika kukarabati majengo yaliyopo ili kukidhi mahitaji na nyenzo za ufundishaji na huduma bora kwa wanachuo na wafanyakazi.

"Pamoja na hatua iliyofikiwa na uongozi wa chuo katika ukarabati wa majengo yapo maombi ya kuendeleza kazi hiyo pamoja na kutafuta ufadhili ya kufanikisha malengo mengine ya chuo", alisema mwenyekiti huyo.

Mkuu wa hicho Dkt. Paul Kihwelo alisema licha ya mafanikio yaliyopo chuoni hapo katika ngazi ya stashahada na astashahada chuo kimeendelea kutekeleza kwa vitendo malengo ya kuanzishwa kwake kwa kutoa mafunzo elekezi kwa watumishi wa mahakama ngazi mbalimbali ikiwemo majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani lakini pia mahakimu wapya.

Dkt. Kihwelo amebainisha kwamba katika miaka ya hivi karibuni chuo kimejiimarisha katika kutoa ushauri (Consultancy) pamoja na utafiti sasa chuo kina miradi kadhaa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments