RAS TANGA ATOA AGIZO KWA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Judica Omari akizungumza wakati wa kikao cha kutangaza matokeo ya wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi mwaka 2020 na kutangaza majina ya wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021.

Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Tanga William Mapunda  akizungumza jambo wakati wa kikao hicho
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhmani Shiloo akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye kikao hicho

Mkurugenzi wa Halamshauri ya Mkinga  Rashidi Gembe kushoto akiwa kwenye kikao hicho
Sehemu ya wadau mbalimbali wakifuatilia kikao hicho kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Kilindi Abeid  na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kilindi, Bw. Gracian MakotaWAKURUGENZI wa Halmashauri mkoani Tanga ambao hawajakamilisha ujenzi wa vyumba avya madarasa wametakiwa kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo ifikapo Februari 28 mwakani.

Agizo hilo lilitolewa leo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Judica Omari wakati wa kikao cha kutangaza matokeo ya wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi mwaka 2020 na kutangaza majina ya wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021.

Alisema kuhusu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi na uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza 2021 huku akieleza wanafunzi wapatao 1,537 hawakuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kutokana na ukosefu wa vyumba vya madarasa katika halmashauri ya jiji la Tanga.

Aidha alisema jumla ya wanafunzi 36,857 sawa na asilimia 96, wakiwemo wavulana 17,546 na wasichana 19,311 wamefaulu na kuchaguliwa kujiunga na elimu ya kidato cha kwanza ifikapo januari 11 mwakani.

“Nitoe wito kwa wakurugenzi ambao hawajachukua wanafunzi wote kusimamia na kuhakikisha madarasa yanakamilika na wanafunzi wote waliobaki wanaanza masomo yao ifikapo tarehe 28 mwezi wa pili 2021 lakini nitoe pongezi kwa wanafunzi wote waliochaguliwa ,viongozi ngazi zote pamoja na walimu,wazazi na walezi”Alisema katibu Tawala Judica.

Hata hivyo alifafanua kuwa kutokana na ufaulu kuongezeka mwaka huu ofisi yake imeshaagiza wakurugenzi wote kufanya maandalizi ya samani zote ndani ya vyumba vya madarsa mapema kwa ajili ya wanafunzi hao.

Alieleza pia idadi ya wanafunzi waliofanya mtihani mwaka huu kwa mkoa wa Tanga walikuwa 53,677 ambao kati yao wavulana ni 25,960 na wasichana ni 27,717 sawa na asilimia 99.27, ambapo aliongeza kuwa waliofaulu kati ya hao ni wavulana 18,284 na wasichana 20,110 na kufanya idadi ya wanafunzi 38,394 sawa na asilimia 71.53.

Katibu Tawala huyo  alisema wanafunzi wapatao 397 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro 325, ugonjwa 14, mimba 36, vifo 19 wanafunzi watatu kwa sababu nyinginezo.

“Napenda kusisitiza kuwa wanafunzi waliopangwa katika nafasi hizi ni wale waliofaulu kwa uwezo wao, iwapo aina yoyote ya udanganyifu ulifanyika na kusababisha wanafunzi hawa wakarudishwa kwa kushindwa kumudu masomo yao, hatua kali zitachukuliwa kwa watakaobainika” alifafanua.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post