DONALD TRUMP AMFUTA KAZI WAZIRI WA ULINZI MARK ESPER | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, November 10, 2020

DONALD TRUMP AMFUTA KAZI WAZIRI WA ULINZI MARK ESPER

  Malunde       Tuesday, November 10, 2020


Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi Waziri wa Ulinzi Mark Esper kuashiria kuwa huenda akatumia miezi yake ya mwisho madarakani baada ya kushindwa kwenye uchaguzi kufanya maamuzi ya kulipiza kisasi katika serikali yake.

 Trump alikuwa amezozana na Esper kuhusu msururu wa masuala na alikasirishwa hasa na hatua yake ya kupinga hadharani vitisho vya Trump vya matumizi ya wanajeshi katika kupambana na maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi baada ya polisi kumuua George Floyd mjini Minneapolis. 

Trump alisema kwenye Twitter kuwa Christopher Miller, mkurugenzi wa Kituo cha Kitaifa Kupambana na Ugaidi, anachukua usukani kama kaimu waziri wa ulinzi. 

Miller, mwenye umri wa miaka 55, amekuwa mkurugenzi wa kituo hicho tangu Agosti. Ni mwanajeshi wa zamani aliyehudumu jeshini kwa miaka 31.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post