BUNGE LA 12 LAANZA KWA KUMCHAGUA SPIKA WA BUNGE | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, November 10, 2020

BUNGE LA 12 LAANZA KWA KUMCHAGUA SPIKA WA BUNGE

  Malunde       Tuesday, November 10, 2020


Mkutano wa kwanza wa Bunge la 12 umeanza leo jijini Dodsoma  wakati Watanzania wakiwa na shauku ya kufahamu nani atateuliwa kuwa waziri mkuu wa Tanzania katika muhula wa pili wa uongozi wa Dk John Magufuli.

Kwa mujibu wa katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai miongoni mwa shughuli zitakazofanywa katika Bunge hilo leo ni kusomwa kwa tangazo la Rais kuliitisha Bunge hilo kwa ajili ya kujadili maendeleo ya wananchi, kutunga sheria mpya pamoja na kuzibadili zilizopo.

Kagaigai alisema baada ya kusomwa kwa tangazo la Rais, utafanyika uchaguzi wa spika na naibu wake, nafasi zinazotetewa na waliokuwapo, Job Ngugai kutoka Jimbo la Kongwa na Dk Tulia Ackson aliyechaguliwa kuwakilisha Mbeya Mjini.

Baada ya uchaguzi huo na spika kula kiapo, wabunge wateule nao, wawakilishi 264 waliochaguliwa majimboni pamoja na 105 wa viti maalumu watano kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wataapa.

Shughuli nyingine kubwa itakayofanyika leo ni kuthibitisha jina la waziri mkuu litakalowasilishwa bungeni na Rais John Magufuli.

Ingawa Rais Magufuli amewahakikishia wateule wa Serikali aliohudumu nao katika miaka mitano ya kwanza kuendelea na nafasi za uteuzi walizokuwa nazo, bado Watanzania wanasubiri kujua kama atafanya mabadiliko yoyote katika nafasi muhimu ya waziri mkuu ama la.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post