TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YATOA SIFA ZA VYAMA VYA SIASA KUPATA WABUNGE WA VITI MAALUM


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera.
***
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema kuwa tayari imeshatoa fomu kwa vyama vya siasa ili kupendekeza majina ya wabunge watakaopata nafasi ya kuwakilisha kupitia viti maalum na chama kitakachopata nafasi hiyo lazima kiwe na asilimia kuanzia 5% za kura za wabunge.

Akizungumza wakati akitoa taarifa fupi ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020, katika hafla ya kumkabidhi cheti mshindi wa kiti cha Urais, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo, Dkt. Wilson Mahera, amesema kuwa chama kitakachopata angalau asilimia 5% ya kura za wabunge kitakuwa na uhalali wa kupata wabunge wa viti maalum.

"Chama kitakachopata angalau asilimia 5% ya kura za wabunge kitakuwa na uhalali wa kupata wabunge wa viti maalum", amesema Dkt. Mahera.

 Via EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post