KATIBU MKUU WA CCM AWATAKA WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI MKUU KUWA NA NIDHAMU NA UWAJIBIKAJI


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi,(CCM), Dk.Bashiru Ally, amewataka viongozi wa chama hicho waliochaguliwa katika ngazi za Udiwani,Ubunge na Wawakilishi kuzingatia nidhamu ya chama na uwajibikaji.

Akizungumza hii leo Novemba 1,2020, Dk. Bashiru, amesema kuwa wanao mfumo kwenye jumuiya zao za chama na kamati za siasa za ngazi zote ambazo zitasimamia na kudai kuwa deni walilonalo ni kuhakikisha wanafanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

''Kwa mara ya kwanza chama chetu kimeingia na kumaliza uchaguzi kikiwa na umoja na mshikamano tukiwa tunaheshimiana na kusimamiana niwaombe wana CCM, wasianze kusherehekea ushindi huu kana kwamba kazi imeisha ila kiukweli kazi ngumu imeanza'',amesema Dk. Bashiru Ally

Aidha amesema siri kubwa ya ushindi walioupata ni umoja wao na kuongeza kuwa ushindi huo ni kutokana na kazi nzuri waliyoifanya katika miaka mitano iliyomalizika.

 Chanzo - EATV


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments