WATAHINIWA 1,024,007 KUFANYA MTIHANI WA KUMALIZA DARASA LA SABA KUANZIA LEO TANZANIA

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk. Charles Msonde, amesema jumla ya watahiniwa 1,024,007 wanatarajiwa kufanya mitihani wa kumaliza darasa la saba ambayo inatarajiwa kuanza leo Oktoba 7 na kumalizima Oktoba 8,2020 nchi nzima.

Pia, Dk. Msonde amewataka wasimamizi wa mitihani hiyo kufanya kazi kwa uadilifu na kulinda haki ya watahiniwa.

“Baraza linatoa wito kwa wasimamizi wote walioteuliwa kwa ajili ya kufanya kazi hiyo, wafanye kwa uadilifu wa hali ya juu na wahakikishe wanalinda haki za watahiniwa wenye mahitaji maalumu”  amesema Dk. Msonde.

Aidha, Dk. Msonde amewataka wamiliki wa shule kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya mitihani, hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote ile kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments