ZITTO KABWE APATA AJALI MKOANI KIGOMA

Chama cha ACT-Wazalendo kimeeleza kuwa kiongozi wa chama hicho, Zitto Zuberi Kabwe amepata ajali ya gari akiwa njiani akitokea Kata ya Kalya kuelekea Lukoma kwenye kampeni katika Jimbo la Kigoma Kusini

Taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari iliyotolewa na Afisa Habari ACT-Wazalendo, Arodia Peter, ilieleza kuwa ajali hiyo ilitokea jana ambapo Zitto alikuwa na watu watano kwenye gari yake.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Zitto na watu hao ote wako salama ingawa walipata majeraha na wanahisi maumivu makali.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba baada ya ajali hiyo walipata huduma ya kwanza kwenye eneo la ajali baadaye walipelekwa Kituo cha Afya cha Kalya kilichopo Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post