MBUNGE MTEULE NEEMA LUGANGIRA AHAIDI KUWAWEZESHA KIUCHUMI VIKUNDI VYA WANAWAKE, WAKULIMA, WAFUGAJI NA WAVUVI


MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira kushoto akizungumza na vikundi vya wanawake katika Kata tatu kwenye Jimbo la Bukoba Mjini
MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na vikundi vya wanawake katika Kata tatu kwenye Jimbo la Bukoba Mjini
MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira katikati (aliyevaa nguo za CCM na miwani) akiwa kwenye picha ya pamoja na vikundi vya wanawake katika Kata tatu kwenye Jimbo la Bukoba Mjini
MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira katikati (aliyevaa nguo za CCM na miwani) akiwa kwenye picha ya pamoja na vikundi vya wanawake katika Kata tatu kwenye Jimbo la Bukoba Mjini
MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira akizungumza na wavuvi ambao hawapo pichani kuhusu namna watakavyoweza kunufaika kupitia sekta hiyo
MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira akizungumza na wavuvi ambao hawapo pichani kuhusu namna watakavyoweza kunufaika kupitia sekta hiyo
MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira akiwa kwenye picha ufukweni mara baada ya kuzungumza na wavuvi
MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira kulia akiangalia ng'ombe wanaofugwa wakati alipokutana na wafugaji
MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira kulia akiteta jambo na mmoja wa wafugaji wakati alipowatembelea ili kubaini changamoto ambazo wanakabiliana nazo na kuona namna ya kuzifanyia kazi


NA MWANDISHI WETU,BUKOBA

MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira ameahidi kwa kuanzia kuwawezesha kiuchumi vikundi vya wanawake katika Kata tatu kwenye Jimbo la Bukoba Mjini

Neema ambaye pia ni Mlezi wa CCM kwenye Uchaguzi huu 2020 kwa Kata hizo Bukoba Mjini aliyasema hayo mara baada ya kutembelea Vikundi vya Kata za Kahororo, Nshambya na Kashai ambapo pia walikubaliana vipaumbele vya uwezeshwaji kiuchumi kwa wanawake wa Manispaa kulingana na Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 inavyosema.

Alisema kwamba lazima vikundi hivyo vitambue fursa zilizopo za uwezeshwaji wamawake kiuchumi kupitia njia mbalimbali ikiwemo mikopo isiyokuwa na riba au riba nafuu sambamba na fursa za elimu ya biashara.

“Lakini pia katika kukutana nao ni kujua kama vikundi vyao vipo hai, vimesajiliwa, changamoto zao za kupata mikopo na namna ya wao kuweza kujikwamua kiuchumi kwa lengo la kuweza kupata mafanikio" Alisema

Hata hivyo pia Mbunge huyo Mteule amekutana na makundi ya wakulima na wafugaji wa Kata hizo pia; Kahororo, Nshambya na Kashai mitano kwa lengo likiwa kupokea changamoto zao ambazo zinawakabili na wakajadiliana kwa kina na kuzipatia ufumbuzi papo hapo kupitia Ilani ya CCM ya Mwaka 2020-2025.

“Lakini pia nimewafuata wavuvi walipo kisiwani na kujadiliana nao kuhusu mageuzi makubwa ambayo Chama Cha Mapinduzi (CCM) inakwenda kufanya kwenye Sekta ya Uvuvi itakayopelekea wavuvi wadogo kunufaika zaidi na sekta yao kama ilivyo kwa wachimbaji madini wadogo" Alisema

 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments