IGP SIRRO AZUNGUMZIA VURUGU ZANZIBAR....ASISITIZA VIONGOZI KULINDA AMANI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, October 27, 2020

IGP SIRRO AZUNGUMZIA VURUGU ZANZIBAR....ASISITIZA VIONGOZI KULINDA AMANI

  Malunde       Tuesday, October 27, 2020
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amewataka viongozi wa siasa, tume na wadau wengine wa siasa kutimiza wajibu wao katika kulinda amani ya nchi wakati huu wa uchaguzi.

“Tunatarajia kumpata rais mmoja atakayechaguliwa na wananchi hivyo kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu wake kudumisha amani iliyopo.”- Amesema IGP Simon Siro leo Oktoba 27 jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa za vikundi vya watu wanaotaka kufanya vurugu.

Ameongeza kuwa jeshi la Polisi limejiandaa kuhakikisha amani ya nchi inaendelea kulindwa huku akiwasisitiza wapiga kura, kwenda kupiga kura bila woga nakuepuka vurugu katika vituo vya kupigia kura. 

Aidha,IGP  Sirro amesema kuna watu 42 waliokamatwa kisiwani Pemba wakidaiwa kuwashambulia polisi waliokuwa wakisambaza masanduku ya kura jana.

"Kama kule Zanzibar, wakati askari wanasambaza masanduku ya kupigia kura, kuna vijana walianza kurusha mawe na wameshulikiwa. Wapo karibu 42. Mpaka sasa hakuna kifo chochote," amesema IGP Sirro.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post