Polisi Zanzibar Wataja Sababu za Kutumia Mabomu Ya Machozi


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi  kisiwani Zanzibar limesema limelazimika kutumia mabomu ya machozi katika baadhi ya maeneo kutokana na uwepo wa viashiria vya uvunjifu wa amani.

Limesema waliokamatwa ni waliochoma matairi na kuyaweka katikati ya barabara na waliokwenda katika vituo vya kupigia kura wakati leo wanaoruhusiwa kupiga kura ni makundi maalum wakiwemo askari wa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na kuyashambulia kwa mawe magari ya polisi.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Oktoba 27, 2020 na Kamanda Polisi wa Mkoa huo, Awadh Juma Haji


Amesema mbali ya matumizi ya mabomu hayo, wanawashikilia baadhi ya vijana waliodai kuhusika katika matukio hayo.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments