IGP SIRRO ATOA ONYO KWA WALIOANDALIWA KUFANYA VURUGU WAKATI WA UCHAGUZI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, October 9, 2020

IGP SIRRO ATOA ONYO KWA WALIOANDALIWA KUFANYA VURUGU WAKATI WA UCHAGUZI

  Malunde       Friday, October 9, 2020


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema hadi sasa wananchi wengi wamekuwa watulivu licha ya kuwepo kwa baadhi ya watu wachache walioandaliwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa kwa ajili ya kufanya vurugu na kujiingiza kwenye uhalifu.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na kuwataka baadhi ya viongozi kufanya masuala ya siasa na kuacha kuwatumia vijana na kuwaingiza kwenye uhalifu na kwamba yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria.

Kuhusu upigaji wa kura Zanzibar, IGP Sirro amesema, wapo baadhi ya watu wanaohamasisha baadhi ya watu au kikundi cha watu kuvunja sheria wakati wa zoezi la upigaji kura kinyume cha sheria, kanuni na taratibu zilizopo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post