DR MAGUFULI AAHIDI KUPANDISHA MISHAHARA KWA WATUMISHI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, October 20, 2020

DR MAGUFULI AAHIDI KUPANDISHA MISHAHARA KWA WATUMISHI

  Malunde       Tuesday, October 20, 2020


Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, Dkt. John Magufuli leo Oktoba 20, 2020, amefanya mkutano katika uwanja wa TTC Korogwe mkoa wa Tanga leo na kunadi sera za chama hicho na kuomba ridhaa ya wana CCM, na wananchi kumchagua kuwa Rais na kuchagua wabunge na madiwani wa CCM.
Akizungumza wakati wa mkutano huo, Dkt. Magufuli ameahidi kupandisha mishahara kwa watumishi iwapo atapewa ridhaa hiyo huku akisisitiza kuwa ili mipango mbalimbali iweze kufanikiwa ni lazima kujipanga kukusanya fedha na kutengeneza miundombinu.

“Maendeleo ni lazima yapangwe, bila kupangwa hakuna kitakachofanyika. Miaka mitano ilikuwa ya kujipanga ndio maana tulijenga  vituo vya afya, zahanati, hospitali za mikoa, rufaa lakini tukaongeza bima, bajeti ya madawa kutoka Sh31 bilioni hadi Sh270 bilioni, hayo yalikuwa maandalizi.

“Uongozi ulio makini ni lazima upange maandalizi, bila hivyo itakuwa ahadi hewa. Ndio maana tulipoingia madarakani tu tuliongeza kukusanya fedha kutoka Sh850 bilioni hadi Sh1.5 trilioni, na hii ndio imetusaidia kujenga reli ya kisasa ambayo tunatumia Sh7.2 trilioni, pia tumeanza mradi wa umeme wa Julius Nyerere,” amesema Magufuli.

Ameongeza, “Miaka mitano iliyopita, tumeajiri watumishi 74,000, tumeimarisha uchumi wetu, sasa miaka mitano ijayo tutakuwa na jukumu la kuongeza misharaha, huwezi kupandisha mishahara wakati huna uchumi, wengine wanazungumza tu hawajawahi kutawala, hata kujenga ofisi za chama zimewashinda."


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post