MREMBO ALIYEDANGANYA MCHUMBA AMEOKOKA ABUGIA KRETI YA BIA KAMA MAJI

Jamaa mmoja nchini Kenya ameachwa mdomo wazi baada ya mwanamke aliyedhani ameokoka kubugia kreti nzima ya pombe chini ya saa mbili baa zilipofunguliwa juzi nchini Kenya. 

Inasemekana kwamba jamaa huyo na mwanamke huyo ambaye ni mpenziwe waliingia baa kula na baada ya kumaliza mlo mrembo aliomba aletewe chupa moja ya pombe. 

 Hata hivyo, kulingana na Taifa Leo jamaa hakukubaliana na ombi la mrembo huyo. “Beib unajua vizuri mimi sipendi kulewa. Tena uliniambia kuwa wewe si mlevi umeokoka. Inakuaje leo unataka pombe?” jamaa alimuuliza mrembo.

 Duru zinaarifu kwamba kipusa alimfungulia roho jamaa na kumfichulia kwamba awali alikuwa akinywa kisha akaacha. 

 “Tulipoanza kuchumbiana niliacha kunywa pombe. Lakini sijui kiu imetoka wapi. Ninataka kuonja tu kidogo,” mwanamke huyo alijitetea. 

Penyenye zinasema kipusa bila aibu alimuagiza weita kumletea mrembo wake chupa moja ambayo aliibugia kama maji. “Beib chupa moja haitoshi. Naomba kuongeza nyingine kwa bill yangu,” mwanamke huyo alimuomba mpenziwe.

 Jamaa alimuagizia chupa zingine mbili ambazo mwanamke huyo aliziporomosha kama maji bila hata kujali.

 “Kwani wewe hii pombe unakunywa aje kama maji,”jamaa alimuuliza mrembo.

 Hata hivyo, mrembo huyo hakujali jamaa alicheka na kumuita mhudumu.

 “Hii pombe yenu ni tamu sana. Leta kreti uiweke hapa. Itakuwa rahisi kwangu kutoa hapa chupa moja moja pole pole badala ya kukuita kila wakati,” mrembo alimueleza mhudumu wa baa.

“Wewe beib, unamaamisha utamaliza pombe hiyo yote?! Mimi sasa nataka kuondoka,”jamaa alimngurumia mrembo.

 Semasema zinaarifu kwamba mrembo huyo alimpuuza barobaro akapanga chupa zote za pombe kwenye meza na kuanza kunywa moja baada ya nyingine hadi kreti nzima ikaisha.

 Inasemekana jamaa aliachwa ameduwaa na kuamka pole pole akashika njia na kuondoka. “Itisha kreti nyingine kama unataka sasa,” jamaa alisema akiondoka. 

Via Tuko News

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments