RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP APELEKWA HOSPITALI BAADA YA KUPATA CORONA


Rais wa Marekani Donald Trump jana amepelekwa katika hospitali ya kijeshi kupatiwa matibabu baada ya kukutikana na ugonjwa wa Corona.

Trump amehamishiwa katika hospitali ya Walter Reed saa 17 baada ya kugunduliwa kuwa na ugonjwa huo. 

Katika vidio fupi aliyoituma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Trump ameonekana akisema kwamba hali yake inaendelea vizuri. 

Msemaji wa Ikulu ya White House Kayleigh McEnany amesema Trump atafanya kazi katika chumba maalum hospitalini kwa siku chache zijazo kama hatua ya tahadhari.

 Inasemekana kwamba Trump mwenye umri wa miaka 74, anasumbuliwa na homa na kwamba atapewa dawa ambayo bado inafanyiwa majaribio. 

Rais huyo wa Marekani wa chama cha Republican amepata ugonjwa wa Corona  akiwa katikati ya kampeni kuelekea uchaguzi wa mwezi Novemba ambapo atachuana na mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden.

 

-DW



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments