VICTOR MKWIZU AAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO YA BARABARA YA MSHIKAMANO KUELEKEA MAKABURINI NGOKOLO

Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge akimnadi Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo Victor Mkwizu (kulia)

Na Suzy Luhende - Shinyanga

Mgombea udiwani kata ya Ngokolo Victor Mkwizu amewaomba wananchi wa kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga wamchague ili aweze kuondoa kero zilizopo ikiwa ni pamoja na barabara ya kutoka Mshikamano kuelekea makaburini katika mtaa wa Mageuzi.

Hayo ameyasema leo wakati akinadi sera zake katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mtaa wa Mageuzi kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga ambapo alisema kero ya barabara inawatesa sana wananchi wa kata ya Ngokolo hivyo aliomba wamchague ili aweze kuiondoa kero hiyo.

Mkwizu amesema barabara hiyo ya kuelekea makaburi ya Mageuzi imekuwa ni tatizo kubwa kwani ikinyesha mvua baiskeli, pikipiki na Magari hayapiti yanakwama njiani wakati mwingine hata magari liyobeba maiti yanashindwa kufika Malaloni hivyo ataliweka kipaumbele kuliondoa tatizo hilo.

 Pia amesema atakapochaguliwa atasikiliza mahitaji mbalimbali ya wananchi katika mataa yote na kuhakikisha anayapeleka sehemu husika ili yaweze kufanyiwa kazi na kutatuliwa.

"Naombeni mniamini ndugu zangu naombeni kura zenu zote kwa Magufuli, kura zenu zote kwa Katambi na kura zenu zote kwa Victor Mkwizu nipeni ili niwawakilishe ili Ngokolo yetu iweze kuwa na maendeleo, ili tutatue kero zote zilizopo",amesema Mkwizu.
Victor Mkwizu akinadi sera zake katika mtaa wa   Mageuzi kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments