MWANAFUNZI WA DARASA LA 7 AJIUA BAADA YA KUKATAZWA KURUDI NYUMBANI USIKU | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, October 17, 2020

MWANAFUNZI WA DARASA LA 7 AJIUA BAADA YA KUKATAZWA KURUDI NYUMBANI USIKU

  Malunde       Saturday, October 17, 2020

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa.
***
Mwanafunzi aliyemaliza darasa la 7 wiki iliyopita katika shule ya msingi Njungwa, Kijiji cha Ngayaki wilayani Gairo, Rahel Yohana (14), amekutwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kanga huku chanzo kikitajwa ni ugomvi kati yake na mama yake mzazi aliyekuwa akimkataza kurudi nyumbani usiku.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, amesema tukio hilo limetokea Oktoba 15 mwaka huu, na akatoa wito kwa wale watu wanaoona njia ya bora ya kutatua changamoto wanazokutana nazo kwenye maisha ni kukatisha uhai wao, kuwa siyo sahihi na badala yake watafute ufumbuzi wa changamoto zao kwa wataalam.

"Aligombezwa na mama yake kwa kosa la kurudi nyumbani mara kwa mara usiku na alitoweka nyumbani na ndipo alipokutwa amejinyonga vichakani, nitoe wito kwa watu ambao wanafikiri 'shortcuts' ya changamoto wanazokutana nazo kwenye maisha ni kuamua kujinyonga, hiyo si sahihi ni bora ukutane na wataalam wa kisaikolojia ili wakusaidie", amesema Kamanda Mutafungwa.

Na mwili wa mtoto huyo mara baada ya kufanyiwa uchunguzi ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post