Angalia Picha : MAELFU WAJITOKEZA KATAMBI AKIWASHUKURU WANANCHI KUMCHAGUA KUWA MBUNGE SHINYANGA MJINI

Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM) akiwashukuru wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwa kumuamini na kumchagua kwa kura za kishindo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28,2020.Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 

Na Damian Masyenene, Shinyanga

Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM) amewashukuru wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwa kumuamini na kumchagua kwa kura za kishindo dhidi ya wapinzani wake, ambapo amewaahidi kuwa hatokuwa mbunge dhaifu na endapo ataenda kinyume na matarajio ya wananchi basi wamuondoe.

Katambi ameyasema hayo leo Oktoba 29, 2020 mchana katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini wakati akiwashukuru wanachama, mashabiki, wakereketwa na wananchi wa jimbo hilo kwa kumchagua kwa kura nyingi jana wakati wa zoezi la upigaji kura.

Katambi alitangazwa mshindi wa ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa kupata kura 31,831 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Salome Makamba wa Chadema aliyeambulia kura 16,608.

Akizungumza na maelfu ya Wana CCM na wananchi waliojitokeza katika mkutano wake huo wa kutoa shukrani kwa wapiga kura, Katambi ameeleza kuwa sasa analo deni kubwa mbele ya wananchi waliomuamini  na kwamba atakwenda kuchapa kazi usiku na mchana.

“Tumefanya uchaguzi wa kihistoria na Shinyanga mmeonyesha mfano, siwezi kutumia nafasi mliyonipa kwa kusaka umaarufu binafsi na mali….ambao hawajanipigia kura wamenipa nafasi ya kuwadhihirishia kwamba mimi ni bora na wakati ujao wataniunga mkono.

“Naomba Mungu anisaidie nikawe kiongozi wa mfano nisije nikawadhalilisha wana Shinyanga, lazima tuelewane mapema atakayetafuna fedha za miradi nitakula nae sahani moja….na nawaomba nikizingua msisite nipigeni chini wekeni mtu mwingine wananchi wanataka maendeleo, na ikitokea diwani hafuati sheria na taratibu za chama na akatumia cheo kwa maslahi binafsi tutampiga chini, lazima tubadilike tulete maendeleo na tuchape kazi,” amesema.

Katika hatua nyingine, Katambi amesema yote yaliyotokea wakati wa kusaka kura yamekwisha na kuwaomba wanasiasa wenzake kuyasahau, ambapo amewasamehe wote waliomtukana na kumdhalilisha, hivyo hivyo akawaomba na wao wamsamehe pale alipowakosea.

“Yeyote aliyenikosea na kunidhalilisha nimemsamehe bure na wote niliowakosea na kuwakera basi wanisamehe pia….pia nawaomba wananchi mtukosoe na kutushauri kwa nia njema ya kujenga, msije mkanisifu tu kunivimbisha kichwa,” ameeleza.

"Nawashukuru sana kwa kunichagua kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, nawapongeza sana kwa sababu hamkuchagua Mbunge Boya 'dhaifu'. Hakika tukishirikiana pamoja tutaibadilisha Shinyanga. Ushirikiano wenu ndiyo nguzo muhimu ya kufikia maendeleo tunayotaka",ameongeza Katambi.

Katambi pia aliongozana na washindi wa nafasi za udiwani katika kata 17 za jimbo hilo, wakiwemo Gulam Hafeez Mkadam wa Kata ya Mjini, Mariam Nyangaka wa Kitangiri, Ruben Masanja wa Lubaga na madiwani wapya ambao wamezikomboa kata zilizokuwa upinzani akiwemo Zamda Shaban wa kata ya Ndala pamoja na Victor Mkwizu (Ngokolo), ambao wamewashukuru wananchi kwa kuwaamini, huku wakiahidi kuwatumikia wananchi na kuibadilisha Shinyanga.

Kwa Upande wake, Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC), Gaspar Kileo maarufu GAKI ambaye alikuwa Meneja Kampeni wa Katambi amewashukuru wananchi wa Jimbo hilo kwa kukiamini Cha Cha Mapinduzi (CCM) kwa kukipa madiwani wote wa kata 17 na Mbunge na kwamba kazi yake ameimaliza kwa mafanikio, sasa anakiachia chama kuhakikisha wateule hao wanatekeleza ilani ya chama hicho kwa vitendo kama walivyoahidi.

Naye Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa akizungumza na maelfu ya wananchi wa Shinyanga kwa njia ya Simu kupitia simu ya Meneja Kampeni Gaspar Kileo amewashukuru wananchi kwa kuendelea kuiamiani CCM na kuchagua wagombea wote.

"Shinyanga Mjini mmetia fora, asanteni sana kwa kuchagua Madiwani wote wa CCM, Mbunge wa CCM na hatuna wasiwasi kuhusu Mgombea Urais Dk. John Pombe Magufuli najua naye mmempa kura za kutosha",amesema Mlowa.

 ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM) akiwashukuru wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwa kumuamini na kumchagua kwa kura za kishindo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM) akiwashukuru wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwa kumuamini na kumchagua kwa kura za kishindo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28,2020.Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM) akiwashukuru wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwa kumuamini na kumchagua kwa kura za kishindo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28,2020.
Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM) na madiwani wa CCM wakiwashukuru wananchi kwa kuwachagua katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28,2020
Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM) akionesha hati ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakari Mukadam
Maelfu ya wananchi wakiwa nje ya Ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini wakimsikiliza Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM) wakati akiwashukuru wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwa kumuamini na kumchagua kwa kura za kishindo dhidi ya wapinzani wake.

Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM) akiwashukuru wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwa kumuamini na kumchagua kwa kura za kishindo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28,2020
Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM) akiwashukuru wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwa kumuamini na kumchagua kwa kura za kishindo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28,2020.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akiwa  amekaa na viongozi mbalimbali wa CCM wakati Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM) amewashukuru wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwa kumuamini na kumchagua kwa kura za kishindo dhidi ya wapinzani wake.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC), Gaspar Kileo maarufu GAKI ambaye alikuwa Meneja Kampeni wa Patrobas Katambi akimpongeza Patrobas Katambi kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga na kumkabidhi kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakari Mukadam (katikati) ili waanze kufanya kazi ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC), Gaspar Kileo 'Gaki' ambaye alikuwa Meneja Kampeni wa Patrobas Katambi akimpongeza Patrobas Katambi kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga na kumkabidhi kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakari Mukadam (katikati) ili waanze kufanya kazi ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubabari Gulam akiwashukuru wananchi kwa kuchagua wagombea wote wa CCM. Kushoto ni Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM).
Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakari Mukadam
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubabari Gulam akimpongeza Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM) kwa ushindi aliopata katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28,2020.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC), Gaspar Kileo 'Gaki' ambaye alikuwa Meneja Kampeni wa Patrobas Katambi akiwashukuru wananchi wa Jimbo hilo kwa kukiamini Cha Cha Mapinduzi (CCM) kwa kukipa madiwani wote wa kata 17 na Mbunge na kwamba kazi yake ameimaliza kwa mafanikio, sasa anakiachia chama kuhakikisha wateule hao wanatekeleza ilani ya chama hicho kwa vitendo kama walivyoahidi wakati wa kampeni.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC), Gaspar Kileo 'Gaki' ambaye alikuwa Meneja Kampeni wa Patrobas Katambi akipokea simu ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa aliyepiga simu Live na kuwashukuru wananchi kumchagua Patrobas Katambi kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga.Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC), Gaspar Kileo ambaye alikuwa Meneja Kampeni wa Patrobas Katambi akimsikiliza Diwani Mteule wa Kata ya Kambarage Hassan Mwendapole  'Anko Mwenda' akiwashukuru wananchi kwa kutekeleza kauli mbiu yake ya Tatu Bila (Kuchagua madiwani,mbunge na Rais wa CCM)
Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC), Gaspar Kileo 'Gaki' ambaye alikuwa Meneja Kampeni wa Patrobas Katambi akimpongeza Victor Mkwizu (kulia) kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Ngokolo iliyokuwa inaongozwa na Emmanuel Ntobi wa CHADEMA . Gaspar Kileo alisema : “Ntobi chaliiiiiiiiii!!!” 
Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas akiwa na Madiwani wateule kutoka kata zote 17 za Jimbo la Shinyanga Mjini wakiwashukuru wananchi kwa kuwapigia kura
Wananchi wakiwa nje ya ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini
Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas akiwa na Madiwani wateule kutoka kata zote 17 za Jimbo la Shinyanga Mjini wakiwashukuru wananchi kwa kuwapigia kura

Maelfu ya wananchi wakiwa nje ya Ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini wakimsikiliza Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM) wakati akiwashukuru wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwa kumuamini na kumchagua kwa kura za kishindo dhidi ya wapinzani wake.
Maelfu ya wananchi wakiwa nje ya Ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini wakimsikiliza Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM) wakati akiwashukuru wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwa kumuamini na kumchagua kwa kura za kishindo dhidi ya wapinzani wake.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC), Gaspar Kileo ambaye alikuwa Meneja Kampeni wa Katambi akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakari Gulam (wa kwanza kulia) wakati Patrobas Katambi akiwashukuru wananchi kumchagua kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.
Maelfu ya wananchi wakiwa nje ya Ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini wakimsikiliza Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM) wakati akiwashukuru wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwa kumuamini na kumchagua kwa kura za kishindo dhidi ya wapinzani wake.
Maelfu ya wananchi wakiwa nje ya Ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini wakimsikiliza Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM) wakati akiwashukuru wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwa kumuamini na kumchagua kwa kura za kishindo dhidi ya wapinzani wake.

Wananchi wakimsikiliza Patrobas Katambi wakati akiwashukuru kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments