CHAMA CHA TLP KIKIONGOZWA NA MREMBA WAMPOKEA NA KUMPA NDIZI NA MBUZI MGOMBEA URAIS WA CCM DK. MAGUFULI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, October 21, 2020

CHAMA CHA TLP KIKIONGOZWA NA MREMBA WAMPOKEA NA KUMPA NDIZI NA MBUZI MGOMBEA URAIS WA CCM DK. MAGUFULI

  Malunde       Wednesday, October 21, 2020
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha mapinduzi CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha TLP Mzee Agustino Lyatonga mrema aliyefika eneo la Himo pamoja na wanachama wachama chake ili kumlaki leo Jumatano Oktoba 21,2020.


Akizungumza mara baada ya Rais kumpa nafasi ya kumuombea kura Mrema amewaambia watu wa Himo na Vunjo kuwa kura zote kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli na ubunge kura ziende kwa Dk. Charles Kimei.

(PICHA NA JOHN BUKUKU-HIMO-KILIMANJARO)
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha mapinduzi CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha TLP Mzee Agustino Lyatonga Mrema aliyefika eneo la Himo pamoja na wanachama wachama chake ili kumlaki leo Jumatano Oktoba 21,2020.
 
Mzee Agustino Lyatonga Mrema pia alileta mbuzi mkubwa pamoja na mkungu wa ndizi kwa ajili ya zawadi ya Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Mweyekiti wa Chama cha TLP akielekea kwenda kumsalimia Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati wanachama wa chama hicho waliposhiriki katika mapokezi ya JPM
Mwenyekiti wa Chama cha TLP Mzee Agustino Lyatonga Mrema akiwa pamoja na wanachama wenzake wakimsubiri Mgombea Urais Dk. John Pombe Magufuli eneo la Himo mkoani Kilimanjaro.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post