MNEC MTEWELE: MCHAGUENI JACKSON KISWAGA NA MADIWANI WOTE WA CCM JIMBO LA KALENGA KWA MAENDELEO

 

Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Teresia Mtewele akimuombea kura mgombea ubunge jimbo la Kalenga Jackson Kiswaga ili aweze kushinda kwa kisindo katika uchaguzi wa mwaka huuMgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha mapinduzi Jackson Kiswaga akieleza kwanini wananchi wa jimbo la Kalenga wanapaswa kumpigia kura nyingi ili awe mbunge wao kwa maendeleo ya jimbo hilo.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Teresia Mtewele akimuombea kura mgombea ubunge jimbo la Kalenga Jackson Kiswaga ili aweze kushinda kwa kisindo katika uchaguzi wa mwaka huu

 
 Na Fredy Mgunda,Iringa.

 
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Teresia Mtewele amewaomba wananchi wa kata ya Kihanga jimbo la Kalenga mkoani Iringa kuwachagua wagombea wanaotokana na chama cha mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kupata maendeleo ya uhakika.
 
Akizungumza kwenye mkutano wa kuwanadi diwani na mgombea ubunge wa jimbo hilo, Mtewele alisema kuwa wananchi wanapaswa kuwachagua wagombea wa chama cha mapinduzi kwa kuwa chama hicho ndio kinaweza kuleta maendeleo tofauti na vyama vingine
 
Alisema kuwa chama cha mapinduzi kimejipanga kuhakikisha kinaleta maendeleo katika kata ya Kihanga kwa kuwa tayari wamejipanga kwa mikakati imara ya kufanya kazi za kimaendeleo.
 
Mtewele alisema kuwa anajua kuwa kata hiyo wanakabiriwa na changamoto ya ukosefu wa huduma za afya kwani hawana kituo cha afya wala zahanati hivyo wakipewa ridhaa ya kuongoza kata hizo watahakikisha wanatafuta ufunzi wa kero hiyo kwa haraka.
 
"Najua kina mama wanajua kukiwa na tatizo kiafya hakuna shughuli za kimaendeleo ambazo zitafanyika kwa urahisi hivyo tupeni miaka mitano hii tuboreshe sekta ya afya kwa kuwa viongozi wa CCM wamejipanga kutatua tatizo hilo"alisema MNEC Mtewele
 
Aidha Mtewele alisema kuwa tatizo la maji kwenye baadhi ya vijiji na vijiji vingine tatizo hill limetatuliwa kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufulu.
 
Alisema kuwa wananchi wa Kihanga wanategemea kilimo kwa kiasi kikubwa hivyo ni lazima kuwasaidia kupandisha thamani ya mazao ili wakulima hao wapate faida ya kilimo hicho.
 
Mtewele alimazia kwa kuwaomba wananchi wa kata hiyo kumchagua mgombea udiwani,ubunge na mgombea urais wa CCM kwa kuwa hao ndio wanaweza kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wa kata na jumbo hilo.
 
Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha mapinduzi Jackson Kiswaga alisema kuwa atakuwa kiongozi wa vitendo na sio maneno kama ilivyokuwa kwa viongozi wengi hivyo wananchi wanapaswa kuchangua kwa kura nyingi ili aweze kuwa mbunge wa jimbo hilo.
 
Kiswaga alisema kuwa wananchi wa kata ya kihanga wanabiliwa na changamoto ya afya,mikopo ya kibiashara na elimu ya ujasiliamali hivyo akipewa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha anatatua changamoto hizo.
 
Aliwaomba wananchi wa kata hiyo kuhakikisha wanakipigia kura zote kwa wagombea wa chama cha mapinduzi kwa ajili ya maendeleo ya jimbo hilo na kata hiyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post