BABA AVURUGA NDOA YA WATOTO WAKE ‘DADA NA KAKA’ WAKIOANA KANISANI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, September 9, 2020

BABA AVURUGA NDOA YA WATOTO WAKE ‘DADA NA KAKA’ WAKIOANA KANISANI

  Malunde       Wednesday, September 9, 2020
Katika hali isiyotarajiwa, Ann Magwi na Jonathan Munini,  kutoka Tana River Kenya, wamelazimika kukatisha zoezi la kufunga ndoa, baada ya James Sidai kujitokeza kanisani na kusema yeye ndio Baba yao Mzazi.


Baba huyo aliingia kanisani akiwa na Dada yake na kusema ndoa hiyo isifungwe kwa kuwa Maharusi ni Ndugu wa damu.

“Mama zenu nyie, mmoja aliniacha akaondoka na mtoto akiwa na mwaka mmoja, mwingine aliona uchumi wangu umeyumba akaondoka akiwa na mimba ya miezi minne na akaolewa na mwalimu, nikaamua kumuoa mwingine na tuna watoto watatu, nimeona tangazo la harusi yenu WhatsApp zile picha nikasema hawa ni wanangu nikachunguza kwa watu mlioishi nao wakasema ni kweli,” amesema James.

Bwana harusi ambaye ni mfanyabiashara katika mji wa Madogo aliondoka kanisani kwa hasira akimuacha mama yake akiwa analia huku bibi harusi akiondoka na mama yake ambaye inadaiwa alikuwa amepoteza fahamu.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post