Picha : MAGUFULI AZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI SHINYANGA..AMFAGILIA KATAMBI, AAHIDI KUMPA KAZI MASELE


Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr John Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi (kulia) wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi CCM mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Septemba 3,2020. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Aliyekuwa Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni za CCM mkoa wa Shinyanga leo .Wa kwanza kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko, Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba na Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timoth Ndanya
Mgombea ubunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akiomba kura
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr John Magufuli akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi CCM mkoa wa Shinyanga.
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr John Magufuli akiwatambulisha wagombea ubunge mkoa wa Shinyanga wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi CCM mkoa wa Shinyanga.
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr John Magufuli akiwatambulisha wagombea udiwani Jimbo la Shinyanga Mjini wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi CCM mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Magufuli, amewaomba wananchi wa Shinyanga kumpa kura mgombea ubunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi ambapo pia ameahidi kumtafutia kazi nyingine aliyekuwa Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele.

Dk. Magufuli ameyasema hayo leo Alhamis  Septemba 03, 2020, wakati akizungumza na wananchi wa Shinyanga mjini katika mkutano wa kampeni za urais uliofanyika katika uwanja wa Kambarage.

“Yale mengine ya pembeni achaneni nayo, Katambi ni kijana nampenda mpeni kura, atawavusha, jana tu nimekutana na Masele aliyekuwa Mbunge wa hapa wala sina tatizo, mimi ni Rais nitamtafutia kazi nyingine, ukishakuwa Rais Makazi yapo mengi tu

“Masele nitamtafutia tu kazi ya kwenda kufanya, ukishakuwa Rais kazi ni nyingi, hata leo kuna nafasi ya Mtu mmoja anafanya hovyohovyo huko, Katambi ameacha Ukuu wa Wilaya Dodoma Makao Makuu kuja kuomba kura Shinyanga anawapenda, Katambi ukichaguliwa usibadilike kama wengine”,amesema Magufuli.

Pamoja na hayo Magufuli ameelezea mipango ambayo anatarajia kuikamilisha katika Mkoa wa Shinyanga iwapo atarejea madarakani baada ya uchaguzi.

“Hapa Shinyanga tumetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa hospitali, zahanati na mradi mkubwa wa kusafirisha umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga ambapo itafika mahali tatizo la umeme litakuwa ni ndoto, kwani tumepeleka umeme katika vijiji 136 vya mkoa huu,” alisema huku akiahidi kukamilisha pia miradi mbalimbali ya barabara mkoani humo.

Mgombea ubunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akiomba kura achaguliwe kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini

Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi CCM Mkoa wa Shinyanga leo.
Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi CCM Mkoa wa Shinyanga leo.
Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi CCM Mkoa wa Shinyanga leo.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527