UMMY MWALIMU ALITIKISA JIJI LA TANGA,AKICHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE WA JIMBO LA TANGA MJINI

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akichukua fomu ya kuomba kuwania nafasi hiyo kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Tanga Daudi Mayeji leo

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akiwaonyesha fomu za kuwania Ubunge Jimbo la Tanga mara baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tanga leo
Umati Mkubwa wa wana CCM waliojitokeza kumsindikiza Waziri Ummy wakati alipofika ofisi za CCM wilaya ya Tanga eneo la Masiwani Jijini Tanga
Waziri Ummy kushoto akiwa na Wabunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga CCM wakati alipokwenda ofisi za CCM wilaya ya Tanga kudhaminiwa na chama chake
KATIBU wa CCM wilaya ya Tanga Salum Kidima akizungumza  
MWENYEKITI wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Mkoba akizungumza 
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa na wananchi na wana CCM wakati alipofika ofisi za CCM wilaya ya Tanga kudhaminiwa



MGOMBEA Ubunge Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu leo amelitikisa  Jiji La Tangawakati alipokwenda kuchukua  fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo hilo huku akiwa anasindikizwa na umati mkubwa wa wananchi na wanachama wa chama hicho.



Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto msafara wake ambao ulikuwa ukisindikizwa na magari, pikipiki huku wananchi wengine wakiwa pembezoni mwa barabara wakimshangilia na kumpungia mikono.



Msafara huo ulizunguka maeneo mbalimbali kwenye Jiji hilo na baadae kufika kwenye ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tanga kwa ajili ya kuchukua fomu za kuwania kiti hicho.



Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu Ummy alisema kwamba anawashukuru halmashauri kuu ya CCM kwa kumwamini na kumpitisha kuwania Ubunge Jimbo la Tanga huku akiahaidi kufanya kampeni za kiistarabu shuka kwa shuka ,kitanda kwa kitanda na uvungu kwa uvungu



Alisema kwa anawashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wilaya ya Tanga ambao walimpitisha kwa kura za kishindo kwa kumpendekeza kuwa mgombea wa Ubunge Tanga mjini .



“Wajumbe wamekuwa ni watu maarufu sana lakini wajumbe wa mkutanbo mkuu wa Tanga mjiniwaoi kwangu mimi wamenitendea haki  kwangu mm wamenipa heshima niwashukuru  sana wenyeviti wa ccm kutoka matawi yote 153 ya jiji la Tanga, makatibu tawi wote, na makatibu wenezi wote pamoja na wajumbe waliotoka kwenye ngazi ya matawi,’’alisistiza Ummy Mwalimu.



Nilipata heshima ya kuwa Mbunge viti maalumu miaka 10 na mshahara wa mbunge wa viti maalumu na jimbo ni mshahara mmoja  ningekuwa nimeshamaliza mchezo lakini kwasababu ya shauku na mapenzi makubwa kwa wanantanga hulka na hamu yangu ya kuipenda Tanga mjini ninataka kuiona yenye heshima na hadhi yake",amesema.



Aidha Waziri Ummy alituma salamu kwa wapinzani wake  kuhakikisha wanajipanga vyema  kwani wao watafanya kampeni za maendeleo  na kampeni za kistaarabu na heshima kampeni zinazoakisi hadhi,utu na heshma yab wanatanga kutokana na hulka ya wanatanga kuwa wastaarabu.



‘’Nitume salamu kwa watani zetu walioingia kwenye kinyanganyiro hiki kuwa sisi tutafanya kampeni za ustaarabu, heshima na maendeleo lakini wakituchokoza …….wataweza kweli..hata wakiungana..matusi kututukana,’’alibainisha Ummy.



Katika hatua nyingine Waziri Ummy alisema watahakikisha wanafanya kampeni za kistaarabu nyumba kwa nyumba, shuka kwa shuka, kitanda kwa kitanda na uvungu kwa uvungu kuhakikisha jimbo linarudi katika chama cha mapinduzi CCM.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527