RAIS MAGUFULI AWASILISHA FEDHA ZA MICHANGO ILIYOTOLEWA KATIKA HARAMBEE KANISANI KUCHANGIA UJENZI WA MSIKITI WA CHAMWINO, DODOMA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, August 24, 2020

RAIS MAGUFULI AWASILISHA FEDHA ZA MICHANGO ILIYOTOLEWA KATIKA HARAMBEE KANISANI KUCHANGIA UJENZI WA MSIKITI WA CHAMWINO, DODOMA

  Malunde       Monday, August 24, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amewasilisha fedha za michango iliyotolewa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Chamwino Mkoani Dodoma.

Fedha hizo zimewasilishwa na Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike kwa Sheikh Mkuu wa Wilaya Suleiman Abdallah Matitu muda mfupi baada ya Swala ya Adhuhuri iliyofanyika katika Msikiti uliopo hivi sasa.

Pamoja na kukabidhi fedha hizo, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza na kuwashukuru watu wote waliounga mkono na wanaoendelea kuunga mkono uchangiaji wa ujenzi wa Msikiti mpya na wa kisasa wa Wilaya ya Chamwino.

Mhe. Rais Magufuli amesema Msikiti huo utajengwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), na ujenzi wake utaanza wiki hii.

Amesema watu mbalimbali wameguswa bila kujali madhehebu ya Dini waliyonayo na kwamba hiyo ni udhibitisho wa umoja na mshikamano walionao Watanzania.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post