Tazama Picha : RAIS MAGUFULI AKILA MHINDI BARABARANI DUMILA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli ameahidi kufanya upanuzi wa barabara na kujenga vibanda vya Wajasiriamali katika eneo la Dumila, Wilaya ya Mvomelo Mkoani Morogoro.Pichani ni Rais Magufuli akila Mhindi wa Kuchoma katika eneo la Dumila Darajani wakati aliposimama kuzungumza na wafanyabiashara hao wadogowadogo akiwa njiani kuelekea Dodoma.(Picha IKULU)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Mhindi wa Kuchoma kutoka kwa mfanyabiashara mdogo katika eneo la Dumila Darajani wakati akielekea mkoani Dodoma.

Wafanyabiashara wa Dumila Darajani wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kusimama katika eneo hilo wakati akiwa njiani kuelekea Dodoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527