CCM KUWASHIKISHA ADABU WAGOMBEA WALIOTOA RUSHWA


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Humprey Polepole

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimesema wale wachache ambao wamekiuka utaratibu wakati wa mchakato wa kura za maoni kwa wagombea wa Chama hicho safari hii watawashikisha adabu na kutashughulikiwa kisawasawa ili iwe fundisho.

Akizungumza leo Agosti 5,2020 jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Humprey Polepole amesema wanao utaratibu wa kikatiba na kikanuni katika mambo yote yanayohusu chaguzi ndani ya Chama hicho

Pia amefafanua mwaka 2016 Chama hicho kupitia vikao vyake kikiwemo cha Halmashauri Kuu na Kamati Kuu viliamua kufanya mageuzi makubwa ya oganaizesheni na uongozi na kukirudisha chama katika mstari.

"CCM kwa sasa tunataka viongozi waadilifu, wachapakazi,wanaochukia rushwa, tutawafundisha watu adabu, hii itakua fundisho kwa wengine, na itabaki kwenye historia kulikua na watu wakubwa tu, lakini tuliwashikisha adabu," amesema.

Polepole amesema wamepokea malalamiko mengi ya vitendo vya rushwa na bado wanaendelea kupokea."Chama chetu kinatambua na kuheshimu, kufuata na kutii bila shuruti kanuni ambazo zinatafsiri sheria ambazo tumejiwekea lakini pia tamaduni, desturi taratibu nzuri ambazo tumejiwekea kwenye nchi yetu." 

Pia amesema kuwa zipo taratibu ambazo zimekubalika hapa nchini na huwa zinatoa mwongozo wa namna wa kutenda na kutenda kwa taifa kwa ujumla, hivyo kama Chama wameanza kufuatilia.

Kuhusu watoa rushwa , Polepole amesisitiza kuwa  watawashikisha adabu. "Wale wachache waliotujaribu, tutawashangaza, tutawashugulikia kisawasawa," amesema Pole pole Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi.

Amesema mwaka 2016 Halmashauri Kuu ya CCM ilifanya mageuzi makubwa ya taasisi na uongozi na kukirudisha chama katika mstari.

"CCM kwa sasa tunataka viongozi waadilifu, wachapakazi, wanaochukia rushwa, tutawafundisha watu adabu, hii itakua fundisho kwa wengine na itabaki kwenye historia kulikua na watu wakubwa tu, lakini tuliwashikisha adabu." amesema Polepole

Amesema wamepokea malalamiko mengi ya vitendo vya rushwa na bado wanaendelea kupokea.

Chanzo - Michuzi TV 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post