NEC YAMTEUA HASHIM RUNGWE KUWA MGOMBEA WA URAIS WA TANZANIA KWA TIKETI YA CHAMA CHA CHAUMMA

Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Semistolces Kaijage kwa mamlaka aliyopewa, amemteua Hashim Rungwe kuwa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mohammed Masoud kuwa mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais kupitia chama cha CHAUMMA.

Rungwe ameteuliwa leo Jumanne tarehe 28 Oktoba 2020 na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage katika ofisi za tume hiyo jijini Dodoma.

Rungwe amekuwa mgombea wa 12 kati ya 17 waliochukua fomu, kurejesha na kuteuliwa na tume hiyo.

Kati ya wagombea hao 12, wawili ni wanawake ambao ni; Qeen Cuthbert Sendiga wa chama cha ADC na Cecilia Mwanga wa chama cha Demokrasia Makini.

Wagombea wengine waliokwisha rejesha fomu na kuteuliwa ni; Rais John Pombe Magufuli (CCM), Leopard Mahona (NRA), John Shibuda (Ada Tadea), Mutamwega Mgaiwa (SAU), Yeremia Maganja (NCCR-Mageuzi), Ibrahim Lipumba (CUF), Philip John Fumbo (DP), Twalib Ibrahim Kadege (UPDP) na Bernard Membe wa ACT-Wazalendo.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527