CHADEMA KUSHIRIKIANA NA VYAMA VINGINE UCHAGUZI MKUU 2020...TUNDU LISSU 'TUKO PAMOJA' | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, August 5, 2020

CHADEMA KUSHIRIKIANA NA VYAMA VINGINE UCHAGUZI MKUU 2020...TUNDU LISSU 'TUKO PAMOJA'

  Malunde       Wednesday, August 5, 2020
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA ambaye ni Mgombea Urais Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema CHADEMA itashirikiana na vyama vingine vya siasa nchini Tanzania katika uchaguzi Mkuu 2020.

Tundu Lissu ameyasema hayo leo kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha ACT Wazalendo unaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam."Tuko pamoja na tutakuwa pamoja,kila mtu amezungumza habari za ushirikiano na nakubaliana na wote waliotaka ushirikiano, tutashirikiana",amesem Lissu. Naye Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Salum Mwalimu ambaye amechaguliwa na chama chake kuwa mgombea Mwenza Urais Tanzania kupitia CHADEMA pia amesema chama hicho kitashirikiana na vyama vingine vya siasa kwenye uchaguzi mkuu 2020.

"Tutakwenda Kushirikiana siyo kuungana kama wengine wanavyosema. Sisi Chadema bega moja lipo ACT Wazalendo,bega jingine lipo CHADEMA tupo tayari kwa ushirikiano.Kazi imeanza na nafikiri tutaimaliza salama",amesema Mwalimu.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post